Kuhusu sisi

Karibu kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo 2025

Sikukuu ya Wakulima ilianza miaka ya 1960 ambapo Serikali ya Tanzania ilianzisha maadhimisho hayo ili kutambua na kuthamini mchango wa wakulima katika uchumi wa Taifa. Maonesho ya Nanenane ni hafla ya kila mwaka inayofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8 kila mwaka ikishirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali zinazohusiana na Kilimo, Mifugo,Uvuvi na Maliasili. Kupitia Maadhimisho hayo, wadau huonesha bunifu na teknolojia pamoja na kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuongeza tija, uzalishaji na uendelevu wa kilimo.

Katika mwaka wa 2025, Tanzania itaadhimisha Maonesho ya 32 ya Nanenane yenye hadhi ya Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza uchumi, kuongeza matumizi ya teknolojia bora na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatafanyika katika Uwanja wa Nanenane Nzuguni katika Jiji la Dodoma, Mji Mkuu wa Serikali. Tukio hili la kifahari linatarajiwa kuvutia washiriki/waoneshaji zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi.